Busha (Hydrocele) ni mkusanyiko usio wa kawaida wa maji kwenye kifuko kinachohifadhi korodani (tunica vaginalis).
Maji hukusanyika kwa sababu ya kutokuwepo kwa uwiano sawa kati ya uzalishaji na utumikaji, kifuko cha korodani kawaida hutoa mil 0.5 za maji kwa siku.
Maji ya busha yana rangi ya majani makavu na hayana uwezo wa kutungisha mimba kwasababu hayana mbegu isipokua yana protini inayozunguka kwa wingi (Albumin), na dutu inayotumika kugandisha damu (Fibrinogen).
MADHARA YA UGONJWA WA BUSHA
Busha linaweza kupelekea mkusanyiko wa damu ndani ya korodani (hematocele).
Ugonjwa wa Busha unaweza kupelekea mkusanyiko wa usaha ndani ya nafasi kati ya tabaka mbili za korodani (Scrotal pyoceles), mara nyingi huambatana na maambukizi ya mishipa ya kuhifadhia mbegu za uzazi (epididymo-orchitis).
Mgonjwa kupoteza uwezo wa kujamiiana na mtu fulani ingawa ana uwezo wa kujamiiana na mtu mwingine (Relative impotency).
Ngiri ya mfuko wa korodani (Herniation of hydrocele sac) huweza kujitokeza na mwisho mgonjwa huteseka kutokana na kuongezeka kwa busha na mara chache busha huweza kupasuka.