Mimba kutishia kutoka (Threatened Abortion) huja na dalili za kutokwa na damu ukeni kabla ya wiki 20 za ujauzito na njia ya uzazi huwa imefunga. Kwa kawaida kutokwa na damu ni kidogo na mtoto anaweza kuendelea kuishi.
Matibabu ya mimba inayotishia kutoka kwanza ni kuthibitisha uwezo wa kijusi kuishi kwa kutumia ultrasound.
Mwanamke anatakiwa kupata muda wa kutosha wa kupumzika, akiwa kitandani nyumbani. Aepuke shughuli za kutumia nguvu ikiwemo kusitisha kushiriki tendo la ndoa.
Muhimu kufika Kliniki mara kwa mara. Hatua za ziada zichukuliwe ikiwa kuna dalili ya kuvuja damu nzito mfano wa nyama za maini, kutokwa uchafu ukeni na maumivu makali ya tumbo.